Thursday, November 2, 2017

Kwa nini Muhammad alioa wake kwa kasi baada ya Khadijah kufa?



Tuongeee iliyo kweli tu jamani.

Muhammad alipomwoa Khadijah, aliishi naye kwa miaka zaidi ya 20 bila kuoa mwanamke mwingine.

Maswali yanayokuja akilini ni:
1.     Je, alipenda sana wanawake walio na umri mkubwa kuliko yeye?
2.     Je, hakupenda ndoa za mitara?
3.     Je, alimheshimu sana au alimwogopa Khadijah?

Tunapotazama katika Sahih Bukhari Juzuu 3, Kitabu 34, Namba 310 tunaamabiwa kuwa siku moja Muhammad alimwuliza Jarir ibn Abdullah:

“Have you got married?"
He replied in the affirmative.
Muhammad then asked, “A virgin or a matron?”
He replied, “I married a matron.”
Then Muhammad said, “Why have you not married a virgin, so that you may play with her and she may play with you?”

Yaani:
“Umeoa?”
akajibu kwa kukubali.
Kisha Muhammad akamwuliza, “Ni bikira au mtu mzima?”
Akajibu, “Nimeona mtu mzima.”
Halafu Muhammad akasema, “Kwa nini hukuoa bikira ili kwamba uweze kuchezacheza na yeye achezecheze na wewe?”

Hii maana yake nini?
Maana yake ni kuwa si kwamba Muhammad alipenda sana kuishi na Khadijah peke yake. Lazima kulikuwa na sababu zingine zilizomfanya aishi naye.

Tukichukulia kwamba Muhammad alikuwa yatima aliyeishi na watu mbalimbali maishani mwake, ni wazi kuwa maisha yake hayakuwa ya uhakika; na bila shaka, akiwa kama kijana, kama ilivyo kwa binadamu yeyote, angetamani kupata mahali pa kudumu pa kuishi.

Kwa hiyo, alipompata Khadijah (maana Khadijah ndiye aliyependekeza waoane), bila shaka Muhammad aliona hiyo kuwa ni fursa hatimaye ya kupata mahali pa kudumu pa kuishi – tena ukichukulia kuwa yeye alikuwa maskini na Khadijah alikuwa ni mwanamke tajiri.

Kwa hiyo, tunaweza kabisa kusema kuwa hakuona mwanamke mwingine kwa sababu yahofu ya kufukuzwa na Khadijah – jambo ambalo lingemfanya arudi kwenye umaskini wa mwanzo.

Kwa nini tunasema hivyo?
Ni kwa sababu mara tu baada ya Khadijah kufariki, ilikuwa ni kama geti la gereza limebomoka.

Muhammad aliweza kukusanya wake wengi, na tunaweza kuamini kabisa kuwa kile ambacho alikuja kumwuliza Jarir ibn Abdullah lazima kilikuwa moyoni mwake siku nyingi. Kwa hiyo, mauti ya Khadijah ilizalisha fursa adimu iliyokuwa imetamaniwa na  moyo wake kwa siku nyingi.

Huenda kuna sababu zingine tofauti na mtazamo wangu.
Nakukaribisha ndugu mwislamu utupe elimu inayohusu jambo hili.

No comments:

Post a Comment