Friday, October 13, 2017

Usidanganyike na ukubwa wa jambo; Uislamu utatoweka kabisa!



Zamani wakati wa Agano la Kale, ziliwahi kutokea falme na mamlaka kubwa zilizotawala dunia nzima ya wakati ule.

Kwa mfano, dola ya mkono wa chuma ya Rumi ilitawala dunia kwa mabavu kwa miaka 1500. Lakini iko wapi leo?

Zimepita tawala nyingi hapa duniani na zingine bado zinaendelea kuja. Na kila utawala UNAJARIBU kuongoza dunia kwa madai kuwa wenyewe ndio unaofaa.


Hata hivyo ni wazi kuwa karibu kila utawala umesababisha mateso tu. Serikali zimeleta mateso kwa watu. Dini zimeleta mateso kwa watu. Siasa, teknolojia, na hata mifumo mifumo mbalimbali kama vile ujamaa, ukomunisti, ubepari, nk – vyote hivyo vimejaribu na kushindwa kuwa syuluhu – badala yake vimekuwa vyanzo vya tabu na mateso ya aina mbalimbali kwa mwanadamu.

Lakini zamani kabla ya Yesu, alitokea mfalme kwenye nchi ya Babeli (Iraki) aliyeitwa Nebukadreza. Aliota ndoto ambayo nabii Danieli anaitaja:

Danieli 2:31-33
Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.


Sanamu hii iliwakilisha tawala mbalimbali za dunia hii. Hizi ni kama mawe yaliyochongwa na wanadamu.


Ndipo Danieli akapewa tumaini la uhakika. Mungu wa mbinguni alimpa ujumbe huu ambao ulikuwa ni kile kitakachotokea baada ya hekaheka za wanadamu.

Danieli 2:34-35
Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

Lilitokea jiwe jingine ambalo halikuchongwa na mwanadamu. Lilisambaratisha falme na tawala na dini na jitihada ZOTE za wanadamu ili kwamba kile kilichotoka kwa Mungu kitawale dunia YOTE milele.


Jiwe hilo ni Yesu Kristo na Ufalme wake.
Mathayo 4:17
Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Uislamu una miaka 1400 sasa. Hata kama utaishi tena miaka 5000 mingine, hiyo ni kama dakika tu mbele ya kipindi kinachoitwa MILELE.
Ubepari utasagwasagwa na kutoshwa na Jiwe la mbinguni.
Umoja wa mataifa utasagwasagwa na kutoshwa na Jiwe la mbinguni.
Umoja wa Ulaya utasagwasagwa na kutoshwa na Jiwe la mbinguni.
UISLAMU UTASAGWASAGWA NA KUTOSHWA NA JIWE LA MBINGUNI.
It’s just a matter of time.

No comments:

Post a Comment