Sunday, April 20, 2014

Je, Yesu Alitumwa kwa Israeli Peke Yake?




Waislamu “wanahubiri” kuwa Yesu  hakuja kwa ajili ya ulimwengu wote bali alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao. Kisha wanasema kuwa Muhammad ndiye mtume sahihi kwa sababu huyo alikuja kwa ajili ya ulimwengu wote. Andiko wanalotumia kupinga utume wa Yesu kwa ulimwengu ni lile alilolisema Yesu wakati akiongea na mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi), ambaye alikuwa anaomba Yesu amponye mwanawe.

Imeandikwa:
Akajibu akasema,  Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:26).


Mungu ni Mungu wa utaratibu na ratiba kamili. Ndiyo maana hakuumba kila mtu kwa mara moja. Alianza na mtu mmoja tu, kisha wengine wote tukatokea kwa huyo mtu. Vivyo hivyo, alianza kwa kujifunua kwa taifa moja tu duniani kote. Kisha kutokea hapo ndipo wokovu unasambaa kwenye mataifa yote. Ni ukweli ulio wazi kwamba, ukiacha Israeli, jamii zote zilizobakia duniani, kwa asili zilikuwa zikiabudu miungu (yaani mashetani). Ni Israeli peke yao ndio ambao kwa asili walianza na Mungu wa kweli.

Ndiyo maana Bwana Yesu alipoongea na mwanamke Msamaria pale kisimani alimwambia hivi:

Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. (Yohana 2:22).


Wokovu unatoka kwa Wayahudi kwa sababu hakuna taifa jingine lolote duniani ambalo lilimjua Mungu wa kweli – yote yalikuwa na dini za kipagani – iwe ni wazungu, Waafrika, Wahindi, Waarabu, n.k. Huo ndio ukweli.

Kusema kwamba Yesu hakuja kwa ajili ya mataifa yote hakuna tofauti na kusema kuwa, kwa vile Mungu alimuumba Adamu na Hawa peke yake, basi Yeye si wa familia yangu maana hakuniumba na mimi kama alivyomuumba Adamu.

Yesu aliongea na wanafunzi wake siku moja na akawaambia kuwa:

Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanzia tangu Yerusalemu. (Luka 24:46-47). 

Je, unaona kwamba Injili inatakiwa kuanzia Yerusalemu? Na je, unaona pia kwamba anasema kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake? Je, mataifa yote ni Israeli peke yake?

Mwanamke Mkananayo alikuja wakati usio wake. Huo ulikuwa ni wakati wa kuhubiri Injili kwa Israeli kwanza ndipo iende ulimwenguni kote.

Ufuatao ni ushahidi zaidi wa maneno ya Bwana Yesu mwenyewe kuthibitisha kwamba alitumwa kwa mataifa yote ulimwenguni na kwamba Yeye ndiye Masihi wa Mungu, yaani aliyepakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu wote.


  • Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. (Matendo 1:8). 
  • Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19).
  • Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. (Yohana 3:17).
  • Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. (Yohana 12:47).
  • Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. (Yohana 10:15-16).
  • Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. (Mat 24:14). 

Nihitimishe kwa kurejea tena mambo machache niliyoyasema. Mungu amekuwa na kawaida ya kuanza jambo na mtu mmoja.


  • Aliumba mwanadamu mmoja, kisha tukatokea humo wote.
  • Alijifunua kwa taifa moja, kisha tukamjua wote.
  • Alianza na Mwana mmoja (Yesu), kisha tunazaliwa wote kwa imani katika huyo.
  • Vivyo hivyo, alileta wokovu kwa taifa moja la Israeli, kisha unasambaa kote – ndiyo maana anasema na mwanamke Msamaria pale kisimani – “Wokovu watoka kwa Wayahudi.” (Yohana 4:22).


Hali hii ya kuanza na mtu au sehemu moja, ni ushahidi kuwa wale wote wanaojifariji kwa maneno eti “dini mbalimbali ni njia tofauti ambazo zote zinaishia kwa Mungu”, wanajidanganya na kupoteza muda wao na uzima wao wa milele! “Wokovu watoka kwa Wayahudi” – yaani KWA YESU PEKEE!


Sasa, kwa kuwa muda wa kusambaa kwa wokovu huo ulikuwa haujatimia (maana Mungu anakwenda kwa ratiba ya majira na nyakati), ndiyo maana akamwambia yule mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi) kuwa hakutumwa ila kwa Israeli.


Lakini utimilifu wa majira ulipofika, yaani alipokufa na kufufuka, tunaona akiwaagiza sasa mitume wake waende ulimwenguni kote.


Na Biblia inasema wazi: Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. (Waefeso 2:11-16).


Tafakari

Hoji mambo

Jiulize

Chukua hatua

13 comments:

  1. somo zuri mtumishi wa mungu ila mbona siku hizi umekua kmya sana. Maki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maki, shalom mpendwa. Asante kwa kutembelea hapa. Ni kweli naonekana niko kimya lakini hata hivyo si kimya ila kuna kona ambayo nimejichimbia. Facebook kuna makundi mengi sana yanayojadili UISLAMU NA UKRISTO. Sasa kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa niko huko tukieneza nuru ya Kristo kwa ndugu zetu.

      Nina shauku sana ya kuwa active kwenye blog na kwa neena ya Bwana sitaacha. Kama una facebook account, unaweza kunikuta kwa jina la jimmy john.

      tunakuwa na mijadala mikubwa sana ambayo mara nyingine inaenda hadi usiku kabisa.

      Bwana akubariki Maki.

      Delete
  2. HAKUNA HATA SEHEMU MOJA NDANI YA BIBLIA MUNGU ANAMWAGIZA YESU AENDE KWA WATU WOTE

    Mr.James, kabla ya kuwatuhumu waislamu, ungeanza kuituhumu biblia yako kwanza kwa sababu hili swala liko wazi kabisa bila ya chenga kwamba Yesu Kristo alitumwa kwa Israel pekee. Tatizo linalokusumbua wewe ni uelewa wa lugha.
    Umesema Mungu kawaida yake anafanya jambo kwa utaratibu maalum na ratiba kamili. Sawa mimi nakubaliana na wewe, lakini umesahau kwamba kila jambo alifanyalo linathibitishwa na yeye mwenyewe kupitia kwa malaika wake au Manabii na Mitume.
    Na pia umesahau kwamba neno la Mungu halitakiwi kuongezwa au kupunguzwa.
    Kumb. 4:2 Msilisogeze neno niwaamurulo wala msipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana Mungu wenu, niwamuruzo.
    Kumb. 12:32 Neno niwaagizalo lolote liangalieni kulifanya, usiliongeze, wala usilipunguze.
    Mith.30:5 Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio. 6 Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
    Sasa ndugu, sikiliza maneno ya Mungu ambayo hayatakiwi kuongeza au kupunguza yanavyosema:
    Mw.17:19
    Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.
    Ndugu, hapa tunapata agano la mungu kwa Isaka kwa ajili ya uzao wa Isaka tu si vinginevyo kwa mujibu wa hiyo haya.
    Kutokana na kauli hiyo ya mungu, tunapata picha kwamba, Yesu kwa kuwa yeye ni kizazi cha Isaka( mt.1:1-17) bila shaka kaja kuendeleza agano lao. Na wale ambao si wa kizazi cha Isaka watafute agano lao ndio maana Yesu aliwakataa na kuwaita mbwa na nguruwe.
    Kwa hiyo Mungu alimtuma Yesu kwa Israeli pekee. (Mt.2:6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli).
    Hii ni kauli ya Mungu mwenyewe, kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba neno la mungu linadhihirishwa.
    Baada ya ahadi ya mungu nini kiliendelea?!!
    Mt.10:5 Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie.6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
    Mdo.5:31 Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.
    Mdo.13:23 Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi;
    Mt.15: 24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie. 26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
    Ndugu, Yesu alipotaja zizi alimaanisha Taifa la Israeli; kondoo ni Wayahudi. Na kondoo wengine ambao si wa zizi lile ni wale Wayahudi ambao walikuwepo nje ya mipaka ya Israeli. Ndio maana tafsiri ya biblia kwa lugha ya kigiriki iliwalenga hao kwa sababu walikuwa hawajui kiebrania.
    “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri injili”haimaanishi kwa watu wote ila, ni kwa walengwa tu! Ukisema kwa watu wote utapingana na mungu na Yesu, kwa sababu hakuna hata sehemu moja ndani ya biblia, mungu anamwagiza Yesu aende kwa watu wote.
    Yoh.17:18 Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni;
    Yoh.17:9 "Mimi nawaombea hao, siuombei ulimwengu bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako, na wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao".
    KWA HIYO YESU ALITUMWA NA MUNGU KUJA ULIMWENGUNI KUWAOKOA WAISRAELI NA YEYE AKAWATUMA WANAFUNZI WAKE WAENDE ULIMWENGUNI KOTE KUWAHUBIRIA WAISRAELI WALIOTAWANYIKA

    ReplyDelete
    Replies
    1. IBRA BADO UPO UPOTEVUNI HADI LEO? KWANZA ULIENDA WAPI SIKU ZOTE HIZO RAFIKI YANGU?

      ANYWAY, KARIBU TENA.

      LAKINI SINA MANENO MENGI KWA HAYA ULIYOSEMA.

      JIBU LAKO NI FUPI SANA

      Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi KWA NJE TU, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; bali yeye ni Myahudi ALIYE MYAHUDI KWA NDANI, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu. (Rum 2:28-29).

      TOKA MWILINI NA UINGIE ROHONI NDIPO UTAJUA BIBLIA INAONGELEA KITU GANI INAPOTA ISRAELI

      TOKA MWILINI UINGIE ROHONI NDIPO UTAELEWA KAZI YA YESU; NA KWAMBA YESU HAKUJA KUANZISHA UTAWALA WA KIDUNIA BALI UFALME WA ROHONI

      (Joh 18:36) Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.

      HOJA YAKO WALA HAINA UHUSIANO KAMWE NA MISSION YA YESU

      Delete

    2. Rafiki yangu James, Mada iliyopo mbele yetu, ni JE,YESU ALITUMWA KWA ISRAELI PEKEE? Mimi nimesema ndio, kwa ushahidi mpana kabisa wa maandiko ya biblia.
      Na tena nikabaini ya kwamba NDANI YA BIBLIA HAKUNA HATA SEHEMU MOJA MUNGU ANAMTUMA YESU AENDE KWA WATU WOTE. Kama unae andiko hilo, tafadhali sana nijulishe ili niweze kubatizwa haraka sana.
      Ndugu, biblia inapotaja Israeli, maana yake ,itategemeana na sentence yenyewe imekujaje.
      Kazi aliyokuja Yesu kufanya mbona ipo wazi tu James!
      Mathayo 15:24 “sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli”. Hii ndio kazi ya Yesu aliejia hapa ulimwenguni kufanya.
      Unajua, ndugu James, Waisraeli katika zama za taurati walipewa utaratibu wa maisha na mungu mwenyewe. Mwz.6:1-25.
      Huo utaratibu ulikuwa wa matendo na imani. Wengi wakapotelewa na imani. Akatumwa Yesu kuja kuwarudisha kwenye mstari.
      2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.
      3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
      4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.yn17.
      USIONGEZE WALA USIPUNGUZE NENO LA MUNGU!!!
      HAKUNA HATA SEHEMU MOJA MUNGU KANTUMA YESU KUJA ULIMWENGUNI KUWAOKOA WATU WOTE!!!

      Delete
    3. shalom! nawashukuru james na ibra katika kumtafuta Mungu wa kweli. James majibu yako ni mazuri sana na sina wasiwasi roho wa Mungu yuko pamoja na wewe. kuitafsiri Biblia ni vigumu sana kiubinadam ila ukiongozwa na roho wa Mungu ni rahisi sana. Yesu mwenyewe anasema roho humuongoza mtu kuijua kweli....
      Lakini yeye atakapokuja huyo ROHO WA KWELI, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
      Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyonayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.(yohana 16:13-115)
      kwa hiyo mimi namuomba roho wa MUNGU amsaidie ibra kuijua ile kweli.
      Hata hivyo YESU mwenyewe alisema ni kwa jinsi gani itachukua mda mrefu watu kumjua Mungu wa kweli. Anasema...
      KUSIKIA MTASIKIA, WALA HAMTAELEWA, KUTAZAMA MTATAZAMA WALA HAMTAONA. MAANA MIOYO YA WATU HAWA IMEKUWA MIZITO, NA KWA MASIKIO YAO HAWASIKII VEMA, NA MACHO YAO WAMEYAFUMBA, WASIJE WAKAONA KWA MACHO YAO, WAKASIKA KWA MASIKIO YAO,WAKAELEWA KWA MIOYO YAO, WAKAONGOKA ''NIKAWAPONYA''.

      Pia James nipo na wewe kabisa ya kwamba alipomaliza kueneza habari njema katika taifa la Israeli aliwatuma wanafunzi waihubiri injili (habari njema ya wokovu) kwa mataifa yote...uthibitisho mwingine wa Biblia akiacha na ule ulioutoa juu ni mafundisho ya petro mwanafunzi wa Yesu....
      ''Petro akafumbua kinywa chake akasema, Hakika natambua ya kuwa MUNGU hana upendeleo,
      bali katika KILA TAIFA mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
      Neno lile aliwapelekea wana wa Israeli, akihubiri habari njema ya amani kwa YESU KRISTO ndiye ''BWANA WA WOTE'' (Matendo10:34-36).
      hapo maandishi yako wazi kabisa kwamba katika kila taifa mtu amchaye hukubaliwa na pia anazidi kusisitiza kuwa YESU ni BWANA wa watu wote.

      HATA hivyo mafundisho ya petro yalithibitika pale waliotahiriwa (waisraeli) na wasiotahiriwa ( wasio waisraeli) ambao wameamini walipompokea ROHO wa MUNGU na kuwashangaza watu...
      Matendo 10: 44-48 inasema..
      Petro alipokuwa akisema maneno hayo ROHO mtakatifu akawashukia watu wote waliosikia lile neo. Na wale WALIOTAHIRIWA, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu MATAIFA nao wamemwagiwa kipawa cha ROHO mtakatifu. kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu. Ni nani awezaye kukataza maji , hawa watu wabatizwe, watu waliopokea ROHO Mtakatifu vilevile kama sisi? Akaamuru wabatizwe kwa jina lake YESU KRISTO. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.

      kwa hiyo ni dhahiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana wa wote wa waisraeli na wa mataifa ndio maana PETRO aliagiza WOTE wabatizwe kwa JINA LA YESU KRISTO.
      Mwenye masikio na asikie.
      Elibarick Andrew....

      Delete
    4. Elibarik, Biblia sio kitabu kigumu kueleweka kama unavyodai wewe. Hizo ni dalili za kushindwa kutetea hoja. Biblia inatakiwa kwa mtu asieamini aisome ailewe na achukuwe hatua. Haijaja kwa ajili ya walioamini tu. Lakini pia, lazima nikubaliane na wewe ya kwamba, kuna sentnsi nyengine za mafumbo ambazo kwa mtoto mdogo sio rahisi kuelewa. Mfano:
      -KONDOO WALIOPOTEA WA NYUMBA YA ISRAELI;
      -SIO VIZURI KUKITWA CHAKULA CHA WATOTO KUWATUPIA MBWA;
      -MSITUPE LULU ZENU MBELE YA NGURUWE, WASIJE KUZIKANYAGA NA KUWARARUA.
      Na kuhusu hii habari ya ROHO WA KWELI, Elibarik utapasuka kichwa.Hautajua chochote, mtabaki mnadanganyana eti ni roho mtakatifu.
      Haya twende sasa! Huyu roho mtakatifu alikuwa wapi wakati Paulo na Barnaba wanapingana?
      Leo hii, kuna makanisa mengi sana hapa ulimwenguni na yote yanapingana. Alikuwa wapi roho mtakatifu wakati mnamegana?
      Kanisa la kwanza limeanza mnamo karne ya IV na lile la Protestant limeanza mwanzoni mwa karne ya XV. Nataka kujua kwanini huyo roho,amechelewa kuwapa watu ukweli au kwanini amewaacha watu wanatoka kwenye kweli?
      Elibarik, akili ni mali. Ukitumia vizuri utafaidika nazo!
      Itabidi ujiulize, hivi ni kitu gani tokea Yesu aondoke hapa duniani chenye sifa za huyo roho wa kweli kimesimama?
      MTUME MUHAMMAD (SAW) ambae amekabidhiwa, KITABU CHA QUR’AN TUKUFU,KITABU AMBACHO 100% NI MANENO YA MUNGU NA NI UONGOFO KWA WANADAMU WOTE ULIMWENGUNI! Ni jibu pekee linalotosheleza kwa ROHO WA KWELI alomsemea Jesus.
      Na hii habari ya kusikia bila kuelewa sijui unamlenga nani, kwa sababu ukisoma katika jibu langu la msingi hapo juu, nimetumia ushahidi wa mungu mwenyewe kuweza kufafanua, ujio wa Yesu hapa duniani. Nimefafanua kwanzia kule ambako imani imeanzia mpaka nyakati za Yesu. Unajua wewe unategemea sana mafundisho ya wanadamu na unaacha ya Mungu. Sasa hiyo ni hatari!
      MATH.15:9 “Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.”
      WAPI NDANI YA BIBLIA MUNGU ANAMTUMA YESU AENDE KWA WATU WOTE?
      Elibarik, injili ilibidi ihubiriwe katika mataifa yote lakini kwa watu maaluum, ambao ni wayahudi. Nilishasema huko juu.
      Na kile kisa cha Petro sio ushahidi wa Yesu kutumwa na mungu kwa watu wote, na kimetoa taswira kwamba kumbe Yesu, hajatoa maagizo kwa wanafunzi wake kuwaendea watu wote ndo maana kilipotokea kile kioja, watu walishangaa. Kwanini wawashangae kama kweli wao waliagizwa waende kwao?
      Yesu si kwa wote, maandiko yako wazi kabisaaaa!!!Uo ni uongo mtakatifu.
      "Mimi nawaombea hao, siuombei ulimwengu bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako, na wote walio wangu ni wako na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao". (YN 17:9).
      Sasa huyu PETRO aliamuru nyinyi mbatizwe, na Yesu Kristo aliwakataeni nani zaidi?
      “Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.” Mth19:28.
      Mmepotea ndugu zangu Wakristo. Mmepewa kristo bandia!

      Delete
  3. Ubarikiwe James kwa neno,pia Matendo ya mitume 2:5 na kuendelea,naamini kabisa kuna baadhi ya watu wa mataifa kama inavyotajwa kwenye matendo 2:9-11 waliamini injili ya Bwana Yesu na walivyorudi makwao naamini hawakukaa kimya waliihubiri injili na ndivyo injili ililvyoanza kuunea katika mataifa

    ReplyDelete
  4. Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake [YOHANA],akasema,Tazama Mwana-kondoo wa Mungu,aichukuaye dhambi ya ulimwengu![Yohana 1:29]

    ReplyDelete
  5. Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake [YOHANA],akasema,Tazama Mwana-kondoo wa Mungu,aichukuaye dhambi ya ulimwengu![Yohana 1:29]

    ReplyDelete
  6. Wewe Ibra huwezi elewa hilo neno kamwe. Maana ujio wa Yesu unatafsiri ambayo kuipata vizuri lazima umvae kwanza roho mtakatifu, lasivyo utaishia kushabikia dini. Na kanisa sio jengo kama unavyojua wewe. Kanisa utalielewa kama utamtafuta yesu na kumjua vizuri. Haleluya!

    ReplyDelete
  7. James ubarikiwe sana kwa neno zr
    Ila kuna watu ambao hawaelewi ni sababu hawana Roho mtakatifu wa kuwafunulia ya rohoni

    ReplyDelete