Monday, January 6, 2014

Maswali yangu kwako Mwislamu




Tarehe 21 Desemba 2012 niliuliza maswali yafuatayo HAPA. Lakini umepita mwaka mzima bado sijapata jibu japo kwa swali hata mojawapo tu! Ina maana maswali haya hayana majibu kutoka kwenye Quran au labda ndugu zangu Waislamu hawajayaona? Of course mimi binafsi najua kuwa hawawezi kuyajibu kwa sababu Uislamu hauna majibu juu ya masuala ya rohoni.

Hata hivyo, ningependa niyaulize kwa mara nyingine tena hapa tunapoanza mwaka huu wa 2014 ili iwe changamoto kwa Mwislamu uwaye yote – ujihoji, ujiulize na ujipime kule uendako.


Swali la Kwanza

 Adamu na Hawa walifukuzwa kwenye Bustani ya Edeni kutokana na dhambi. Sisi pia tulio uzao wao ni wenye dhambi? Suluhisho la tatizo hili ni moja tu kulingana na Biblia – Yesu Kristo alikufa msalabani na kufanyika sadaka au dhabihu ili sisi tusiendelee kuchinja wanyama kila siku kwa ajili ya dhambi zetu kama torati inavyosema, badala yake tuamini TU katika sadaka ya Yesu na kupokea msamaha wa dhambi na wokovu wa Mungu bure.


Waislamu hamumwamini Yesu Kristo kama mwokozi aliyefia dhambi za wanadamu wote. Je, suluhisho la dhambi kwa mwanadamu ni nini? Kwa maana nyingine, ninyi Waislamu mtaponaje na jehanamu ya moto ilhali ni wazi kuwa ninyi, kama ilivyo kwa kila mwanadamu, mna dhambi ambazo ndizo hizohizo zilimtenga Adamu na Mungu?

Swali la Pili
Biblia inasema: Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:8-9). Kwa hiyo mimi Mkristo nikijikuta nimetenda dhambi nakwenda mwenyewe kwa Bwana Yesu na kumwambia, “Bwana wangu, nimesema uongo, nimeiba, nimetukana, nimetamani, … n.k. naomba unisamehe.” Sisubiri hadi mchungaji au mtu mwingine anikamate kwenye kosa kama polisi wanavyokamata wahalifu.


Ninyi Waislamu mnasema kuwa torati ndiyo njia sahihi ya maisha ya mwanadamu, kwamba mtu akifanya makosa ni lazima aadhibiwe kama vile kupigwa mawe, kuchapwa viboko, kukatwa mikono, n.k. 



Swali ni kuwa, kwa nini hatusikii Waislamu wakijipeleka wenyewe kupokea adhabu hizo baada ya kufanya dhambi? Hatujawahi kusikia Mwislamu ameenda kusema, “Jamani nimezini kwa hiyo nimekuja mnipige mawe; Nimeiba, hivyo nimekuja mnikate mkono.” Kwa nini wanaoadhibiwa ni wale TU wanaokamatwa? Mnataka kutuambia kuwa wakosaji ni hao tu? Kama unaamini kuwa mzinzi ni lazima apigwe mawe, si uende ukaombe wakupige mawe baada ya kuzini. Kwa nini hamfanyi hivyo?


Swali la Tatu
Huenda katika swali la hapo juu utajitetea kwa kusema huendi kwa sababu hujakamatwa (ingawaje Mungu tayari anakuwa ameshakukamata). Sasa, mbona hatusikii mkiwapiga viboko mia, au kuwakata mikono watoto wenu wenyewe kwenye familia zenu pale wanapoiba mboga au fedha nyumbani?


Bila shaka wizi ni wizi tu hata kama aliyeufanya ni mtoto. Ndiyo maana huwa tunawachapa viboko kwa namna ya kawaida isiyo ya kidini. Kwa nini basi sheria za kiislamu zinakuwa sahihi pale zinapohusu tu watoto wa wengine?


Swali la Nne
Hivi ni mwanadamu gani anayeweza kusema kuwa anaweza akae japo siku moja bila kutenda dhambi? Au hata nusu siku? Au hata saa moja tu? Hivi kuna mtu anaweza kuoga mara moja kwa mwezi halafu akabaki safi kwa mwezi huo mzima? Mimi naamini hilo haliwezekani. Ukitaka kuwa safi ni lazima uoge kila siku. Sasa, kama ambavyo jasho, vumbi na harufu mbaya ni uchafu wa mwili, je, dhambi si ndiyo uchafu wa roho? Na kama dhambi ni uchafu wa roho, “logic” ya ninyi Waislamu kuwa na mwezi mmoja wa toba ni nini? Unawezaje kutubu kwa mwezi mmoja halafu eti uwe safi mwaka mzima?


Swali la Tano
Bila shaka ninyi mnaamini kabisa kuwa Uislamu ni dini inayowapeleka mbinguni. Pili, mnaamini kuwa mtu akijitoa muhanga kuua makafiri (yaani akifa huku anatetea dini ya Mwenyezi Mungu), anakwenda peponi moja kwa moja.


Na bila shaka mnaamini kuwa wale makafiri wanaouawa na mwislamu kama huyo wanakwenda motoni, maana hata hivyo, wao si ni maadui wa Allah na dini yake?


Tuchukulie kuwa una watoto watatu – Amri, Hemedi na Sauda. Amri anakuja kwako na kusema, “Baba, Hemedi na Sauda wamekataa kufua nguo kama ulivyosema. Kwa hiyo nimewaua.”


Hivi, ni mwislamu gani atakayesema, “Safi sana mwanangu. Wewe ndiye unayefaa kabisa kuwa mwanangu.”


Mungu ameumba waislamu pamoja na makafiri ambao “hawataki kufua” – yaani hawataki kushika dini yake. Lakini kuna waislamu leo wanatarajia kuwa baada ya kufa, labda watamwendea Mungu huyu aliyewaumba wanadamu wote, na kusema, “Baba, nimeua makafiri mia moja kwa sababu walikuwa hawataki kufuata dini yako” – ambao maana yake ni kuwa hao mia moja wameenda jehanamu ya moto.


Kwa maneno mengine, mwislamu huyu anachomwambia Mungu hapo ni hiki: “Baba, nifungulie mlango wa pepo mimi kiumbe wako mmoja maana nimepeleka viumbe wako mia moja jehanamu.”


Swali ni kwamba: Inawezekanaje wewe ukaenda mbinguni kutokana na kupeleka wengine jehanamu? Tena wale mia moja ni watoto wa baba yuleyule unayemwomba akufungulie mlango wa mbingu!


Swali la Sita
Kama Mungu aliumba mbingu na nchi na kila kitu kwa neno lake tu, iweje leo neno lake hilohilo lishindwe kubadili tabia tu za watu hadi Uislamu ulazimishe kwa nguvu ya upanga kuliingiza neno hilo ndani ya wanadamu? Kwa nini nchi za Kiislamu kama vile Iran, Saudi Arabia, n.k. zina polisi na mahakama kwa ajili ya kuzuia watu kutenda dhambi!!!!! Yaani polisi wanapita huku na kule kuhakikisha watu hawazini, hawalewi, n.k. Ajabu mno! Hivi ni kweli Allah anaweza kusema kwa ujasiri kwamba watu katika nchi hizo wanampenda? Si kwamba watu kama hao wanaogopa tu polisi na mahakama? 


Hata hivyo, wanachofanya polisi ni kuzuia watu kutenda dhambi kwa nje. Je, moyoni inakuwaje? Au hamjui kwamba wizi, uzinzi n.k. haukai mwilini bali moyoni? Maskini wee! Mbona Mungu wenu kawaacha mnahangaika peke yenu? Mnahangaika kutafuta waumini kwa kutumia upanga! Mkishawapata mnahangaika kuwalinda kwa polisi na mahakama ili wasitoke! Mnahangaika kuzuia dini zingine kuhubiriwa kwenye nchi za Kiislamu ili watu wasijui ukweli utakaowafanya wauache Uislamu! Kweli ndugu zangu mnatia huruma kupita kiasi.


Swali la Saba
Kama Uislamu ungekuwa na neno la kweli, kwa nini nchi za kiislamu zinaogopa na kupiga vita kabisa Ukristo kuhubiriwa humo? Je, hii si ishara kuwa mnafahamu kuwa watu watajua kweli ambazo zitawafanya waukimbie Uislamu?
Jiulize
Jihoji
Jipime
Chukua hatua

6 comments:

  1. kaka james, una maswali mengi sana. ngoja nikurupuke na maswali yako
    1. swali la kwanza:
    kila mtu ataubeba mzigo wake. hakuna aliyeletwa duniani kuja kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi ya wengine. haiingii akilini kwamba raha ya kuzini na mwanamke uipate wewe james , kisha yesu aje ateswe. kwetu sisi mtu kwanza anatakiwa ajue kuwa katenda dhambi, ajijutie yeye mwenyewe, amuombe allah msamaha na kisha anuie kutokurudia dhambi hiyo na kutekeleza ibada zote alizoagizwa na allah.

    swali la pili:
    kwanza huwa mnafanya makosa sana kumuomba yesu au kutubia kwa mapadre kanisani, kwan anayepaswa kutubiwa ni muumba peke yake. pia sheria za kiislam hazitekelezeki hapa tanzania kwa kuwa sheria za kikafir zimetubana na hivyo kumuachia muumba mwenyewe aukumu. pindi tutakapo tekeleza japo moja ya kuua basi tunaishia jera. na ndio maana tumeomba mahakam ya kadhi ww mwenyewe unaona mpaka leo bado hatujapewa.

    swali la tatu:
    nafikir linafanana na la pili, sheria ya kikafir imetunyima uhuru.

    swali la nne:
    hakuna siku ambayo sio ya toba, kila siku na kila muda wa swala kwa swala tano kwa siku na swala za usiku huwa tunafanya toba. ila tumeutukuza mwezi wa ramadhani kama alivyo utukuza muumba wetu. ni sawa na wakristo kipindi za kwaresma au majilio. hapa huna swali ila unajiurudisha tu

    swali la tano:
    kama kafir akiamua kutenda dhambi binafsi bila kuiletea athar dini ya allah haina shida tutamuelimisha tu, ila kama anafanya njama za kuusambaratisha uislam, tunabidi tumsambaratisha ili kuinusuru dini ya allah nasi tukawe na lakujibu insha allah. makafir siku zote hupanga njama za kuidhofisha uislam.

    swali la sita
    allah katuambia kuwa tukiona maovu yanafanyika, njia tatu za kuyaondoa.1. kulitoa kwa mkono, 2. kulikemea au ukishindwa kabisa basi kulichukia. acha watekeleze amri yake muumba na sio yako.

    swali la saba:
    yaan kilichoitajika ni kuuondoa kabisa ukafir, kwan una hira sana na wanamatendo machafu sana kutokana na mila zao za kipagani. mf. mavaz, vyakula vya halam nk. so kama kuna nchi inaendeshwa kiislam dhair kuwa ukristo hautakiwi kabisa. watanzania tumeshindwa coz ndo tumetawaliwa ila ipo siku allah atatupa uwezo wa na atatunusuru insha allah.

    nimeamua kujibu kwa ufupi ila utakapoendelea tutajibizana kwa maandiko.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swali la 1 umejibu: kila mtu ataubeba mzigo wake. hakuna aliyeletwa duniani kuja kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi ya wengine. haiingii akilini kwamba raha ya kuzini na mwanamke uipate wewe james , kisha yesu aje ateswe. kwetu sisi mtu kwanza anatakiwa ajue kuwa katenda dhambi, ajijutie yeye mwenyewe, amuombe allah

      .............................
      Nianze kwa kukushukuru Oscar kwa kujitokeza kujibu maswali haya. hii inatusaidia kupata ufahamu juu yay ale tusiyoyajua. Lakini pia niseme kuwa jibu lako halina ukweli wala uhalisia.

      Hivi tuseme hujawahi kusikia kuwa mtu amekamatwa na polisi na anatakiwa kwenda rumande lakini kama ikipatikana dhamana anaachiwa? Je, kumlipia mtu dhamana ni nini kama si kubeba kosa lake.

      Kwa watu au familia zinazotawaliwa na upendo hili ni jambo la kawaida sana. Upendo hutuwezesha kubeba makosa ya wengine. Of course upendo si msamiati ulio katika lugha ya Allah ndiyo maana unapata shida na ushangao. Na hilo linaeleweka.

      Mungu wa kweli, yaani Yehova, ni Baba yetu (na pia Baba yako japo humtaki). Sisi ni sehemu ya familia yake. Anatupenda na yuko tayari kutusaidia katika madhaifu yetu. Ndiyo maana Bwana Yesu anasema: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” (Mathayo 11:28).

      Yakriban miaka 700 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo, Mungu kupitia nabii Isaya alisema yafuatayo [zingatia zaidi maneno niliyoandika kwa herufi kubwa]:

      Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. HAKIKA AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU, AMEJITWIKA HUZUNI ZETU; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, ALICHUBULIWA KWA MAOVU YETU; ADHABU YA AMANI YETU ILIKUWA JUU YAKE, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; NA BWANA AMEWEKA JUU YAKE MAOVU YETU SISI SOTE. Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; ALIPIGWA KWA SABABU YA MAKOSA YA WATU WANGU. Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake. Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; UTAKAPOFANYA NAFSI YAKE KUWA DHABIHU KWA DHAMBI, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake; Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake; Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; NAYE ATAYACHUKUA MAOVU YAO. (Isaya 53:2-11).

      Huyu ndiye Baba anayeijali familia yake. Lakini Allah yeye anasemaje? Piga! Ua! Chinja! Kata vichwa! Kata mikono! Baka wanawake wao! Halafu anawangoja na mizani yake ya kupimia matendo mema na mabaya. Na tuseme hayo hapo juu ndiyo matendo mema yenyewe, siyo?

      Anyway, nihitimishe tu kwa kusema, SI KWELI HATA KIDOGO kwamba mtu mwingine hatakiwi kuteseka kwa ajili ya mwingine. [Ila kwa Allah hiyo ni sawa kabisa].

      Delete
    2. Swali la 2 umejibu: kwanza huwa mnafanya makosa sana kumuomba yesu au kutubia kwa mapadre kanisani, kwan anayepaswa kutubiwa ni muumba peke yake. pia sheria za kiislam hazitekelezeki hapa tanzania kwa kuwa sheria za kikafir zimetubana na hivyo kumuachia muumba mwenyewe aukumu. pindi tutakapo tekeleza japo moja ya kuua basi tunaishia jera. na ndio maana tumeomba mahakam ya kadhi ww mwenyewe unaona mpaka leo bado hatujapewa.

      .....................................

      Mimi sijauliza kuhusu Tanzania. Kwani siku mkipata hiyo mahakama ya kadhi ninyi ndio mtakuwa nchi ya kwanza ya kiislamu? Kama unadhani ninyi hamfanyi hivyo kwa vile mnabanwa na sheria za kikafiri kama unavyodai, basi onyesha ni kwenye nchi gani ya kiislamu hapa duniani – iwe ni Iran, Saudi Arabia, n.k., ambako wazinzi hujipeleka wenyewe wakapigwe mawe?

      Na tena, kwani kama ikitokea mkawa na hizo sheria zisizo za kikafiri, je, iko sheria inayokutaka ukajisalimishe kwa wapiga mawe pindi unapozini?

      ......................................

      Swali la 3 umejibu: nafikir linafanana na la pili, sheria ya kikafir imetunyima uhuru.

      ............................
      Hapa pia hujajibu swali kwa kusingizia kuwa kunyimwa uhuru (typical Islamic spirit, eh Oscar? – kulalamika na kunung’unika). Kama ilivyo kwa hilo swali lililotangulia, onyesha mfano kutoka kwenye nchi za kiislamu – si zipo? Tueleze kuwa Saudi Arabia mtoto akiiba mboga, baba au mama yake anampiga viboko mia; au hata hamsini?

      .............................

      Swali la 4 umejibu: hakuna siku ambayo sio ya toba, kila siku na kila muda wa swala kwa swala tano kwa siku na swala za usiku huwa tunafanya toba. ila tumeutukuza mwezi wa ramadhani kama alivyo utukuza muumba wetu. ni sawa na wakristo kipindi za kwaresma au majilio. hapa huna swali ila unajiurudisha tu

      ...................................

      Nianze kwa nukuu hii: ” Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Mwenye kufunga Ramadhani akiwa na imani na akawa na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allah DHAMBI ZAKE ZOTE ZILIZOPITA husamehewa, Na mwenye kusimama kwa swala (tarawehe) katika mwezi wa Ramadhani akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo (kutoka kwa Allah), DHAMBI ZAKE ZOTE ZILIZOPITA zitasamehewa. Na yule atakayesimama (kwa swala) katika usiku uliobarikiwa (Lailatul-Qadri) akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allah (s.w.) DHAMBI ZAKE ZOTE ZILIZOTANGULIA zitasamehewa. (Bukhari na Muslim).”

      Sasa wewe Oscar unasema kuwa kila siku ni siku ya toba, je, maana ya DHAMBI ZILIZOPITA au ZILIZOTANGULIA ni nini katika nukuu hiyo hapo juu?

      Delete
    3. Swali la 5 umejibu: kama kafir akiamua kutenda dhambi binafsi bila kuiletea athar dini ya allah haina shida tutamuelimisha tu, ila kama anafanya njama za kuusambaratisha uislam, tunabidi tumsambaratisha ili kuinusuru dini ya allah nasi tukawe na lakujibu insha allah. makafir siku zote hupanga njama za kuidhofisha uislam.

      ……………………………………..

      Mimi nimekupa mfano wa familia. Nilitegemea baada ya maelezo yako ungehitimisha kwa kuniambia pia hivi, “Kama mwanangu akija kuniambia ameua ndugu yake ambaye hataki kunitii mimi mzazi wake, nitafurahi kwelikweli.” Au siyo Oscar. Na kama hufanyi hivyo, basi maana yake ni moja tu – wanadamu wana hekima kuliko Allah!

      Ndugu, uislamu ni “utopian” life; yaani ni maisha ya kufikirika tu yasiyo na uhalisia wowote. Na ndiyo maana inabidi uwe na hasira, chuki na ukatili ili kuyatekeleza – kwani katika hali ya kawaida hayatekelezeki.

      ……………………………………….
      Swali la 6 umejibu: allah katuambia kuwa tukiona maovu yanafanyika, njia tatu za kuyaondoa.1. kulitoa kwa mkono, 2. kulikemea au ukishindwa kabisa basi kulichukia. acha watekeleze amri yake muumba na sio yako.

      ……………………………………….
      Nashukuru kwa kuwa unadhihirisha wazi kuwa neno la Allah halina uwezo wa kubadili hali ya mambo ndiyo maana anahitaji sana support ya mkono wa mwanadamu (kulitoa kwa mkono). Sasa kama hivyo ndivyo, wa nini Mungu kama huyo?

      Hebu pata kionjo kidogo juu ya Mungu wa kweli, Oscar: “Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?” (Yeremia 23:29).

      Huyu ndiye Mungu wa kumfuata. Neno tu! Neno tu! Neno tu! Panga la nini? Chuki ya nini? Hasira ya nini?

      Uislamu upo kulingana na ‘the law of the jungle’, yaani ‘survival for the fittest’. Maana yake ni kuwa unajitahidi kupanda juu ya wengine kadiri uwezavyo ili wewe uende juu (peponi) na wao waende chini (kuzimu). Kwamba eti unaua kafiri halafu unapata swawabu na kuingia peponi!!!

      Hapo juu ulisema kuwa haiingii akilini kwamba mtu aadhibiwe kwa dhambi za mwingine. Kama unatafuta amacho hakiingii akilini, basi ndio hiki haswaa!

      Delete
    4. Swali la 7 umejibu: yaan kilichoitajika ni kuuondoa kabisa ukafir, kwan una hira sana na wanamatendo machafu sana kutokana na mila zao za kipagani. mf. mavaz, vyakula vya halam nk. so kama kuna nchi inaendeshwa kiislam dhair kuwa ukristo hautakiwi kabisa. watanzania tumeshindwa coz ndo tumetawaliwa ila ipo siku allah atatupa uwezo wa na atatunusuru insha allah. nimeamua kujibu kwa ufupi ila utakapoendelea tutajibizana kwa maandiko.
      …………………………………
      Oscar acha kunichekesha. Ndiyo maana nimekuambia kuwa uislamu ni ‘utopian life’. Kwamba eti wasio waislamu, yaani makafiri, wana matendo machafu sana. Quran inasema hivi: “Wale wasioamini miongoni mwa Watu wa Kitabu na wapagani wataungua milele katika moto wa jehanamu. Hao ni waovu kuliko viumbe wote. Lakini wale wanaoikumbatia imani na kutenda mema ni waadilifu KULIKO VIUMBE WOTE.” (Al-Bayyina 98:6-7).

      Hebu niambie; unaelewa nini na maneno KULIKO VIUMBE WOTE? Maneno haya yanaonyesha kuwa Quran ni bora zaidi au Biblia ni bora zaidi? Kama swali hili ni gumu kwako, niulize tu nitakwambia jibu lake.

      Delete
  2. Nimefatilia mjadala huu kwa muda mrefu sana, waungwana ningependa nipate namba ya Ibrabura, mafundisho yake y ukweli. happysteven007@hotmail.com

    ReplyDelete