Sunday, March 17, 2013

Maswali Yanayonitatiza Kuhusiana na Quran



Ibra na Waislamu wengine, kumekuwa na kawaida kwa ulimwengu wa Kiislamu kufanya kila juhudi kuonyesha kwamba Biblia imepotoshwa, ingawaje jambo hilo si kweli hata kidogo. Ukiachilia mbali makosa ya kibinadamu ya hapa na pale ambayo yanaingia kutokana na ukweli kwamba Biblia imetafsiriwa na inaendelea kutafsiriwa mara nyingi sana, hakuna makosa ya makusudi yanayofanywa ili kupotosha au kuficha ukweli.

Na juhudi hizi zote zinafanywa ili kutaka kuonyesha kwamba  Quran ni neno la Mungu la kweli ambalo halijapotoshwa hata kidogo. Basi mimi naomba mnisaidie majibu ya maswali haya machache kati ya mengi:

1.  Sura 54:19 inasema kuwa mji wa Aad uliharibiwa kwa siku moja na sura 69:6,7 inasema kuwa uliharibiwa kwa 'usiku' sita na siku nane (seven nights and eight days). Hapo kuna mkanganyiko au la?

2.  Sura 19:17 inaonyesha kuwa malaika alimtokea Mariamu lakini sura 3:42 inasema walikuwa malaika wengi.

3.  Sura 28:40 inasema kuwa farao alizama na kufia kwenye maji lakini sura 10:92 inasema kuwa farao huyo alipona.

4.  Sura 18:86 inasema kuwa jua huzama kwenye chemchemi ya maji yenye tope. Unadhani hii ni sahihi. Jua lina joto la zaidi ya nyuzijoto 6000 kwenye uso wake. Lakini maji yakifika nyuzijoto 100 yanageuka mvuke. Je, maji yanayotajwa kwenye sura hii ni maji gani? Unadhani ni Mungu aliyeumba jua na maji ndiye anayesema haya?

5.  Sura 15:19 inasema kuwa dunia ni bapa kama meza (flat). Kama Mungu ndiye aliumba dunia na ndiye alileta Quran, anaweza kusema jambo kama hili?

6.  Sura  86:6,7 inasema kuwa manii ya mwanamume hutokea kati ya uti wa mgongo na mbavu. Hii ni sayansi ya wapi? Ni kutoka kwa Mungu aliyeumba wa mbingu na nchi na uti wa mgongo na mbavu kweli? Kama haitoki kwa Mungu basi hata kitabu chenyewe nacho hakitoki kwa Mungu, au siyo?

7.  Sura 19:27,28 inasema kuwa Mariamu alikuwa ni dada wa Haruni. Lakini tangu Haruni aishi ilipita miaka 1300 ndipo alipozaliwa Mariamu. Ni Mungu gani basi anayeweza kusema maneno kama haya?

8.  Sura 28:8 inasema kuwa farao na Hamani waliishi wakati mmoja na mahali pamoja. Lakini historia iko wazi kwamba kuna tofauti ya miaka takribani 1000 kati ya watu hawa. Vilevile, farao aliishi Misri wakati Hamani aliishi Uajemi kwenye ngome iliyoitwa Shushani.


MAONI YANGU

Biblia na Quran zote zina makosa fulanifulani ya kibinadamu yalioyoingia humo wakati wa kuandikwa kwa vitabu hivyo. Kwa upande wa Biblia (sijui sana upande wa Quran), huwa nakutana na makosa kadhaa, kwa mfano kukosewa kuandikwa kwa neno, kutafsiriwa vibaya kwa neno, kukosewa kwa takwimu, n.k. Mimi nadhani kuwapo kwa makosa ya aina hii si ishara kwamba kitabu hiki hakitoki kwa Mungu. Ingekuwa ni kweli kwamba makosa haya yaliingizwa ili kuficha au kupindisha ukweli fulani, basi huko ndiko kungekuwa ni kupotosha maandiko.

Kwa upande wangu kipimo kikuu cha kutambua iwapo neno fulani ni la Mungu au la, ni MAFUNDISHO ya Mungu anayehusika.  Kwa mfano, hapo juu nimetoa mfano wa Sura 54:19 inayosema kuwa mji wa Aad uliharibiwa kwa siku moja ilhali sura 69:6,7 inasema kuwa uliharibiwa kwa 'usiku' sita na siku nane (seven nights and eight days). 

Mimi sioni kama hiki ni kigezo cha kusema kuwa Quran si kitabu cha Mungu wa kweli. Au aya moja kusema farao alizama maji na nyingine ikasema hakuzama. Aina hii ya ukinzani kwangu si kigezo cha kubatilisha kitabu.

Lakini tunapoenda kwenye mafundisho yanayohusu mwenendo wa kuishi na wanadamu wenzako, vigezo vya utakatifu, wajibu wa muumini kwa Mungu, wanadamu wenzake na jamii kwa ujumla, n.k., hapo ndipo ninaona kuna uwezekano wa kutenganisha kati ya ujumbe wa Mungu wa kweli na usio wa Mungu wa kweli.

Kama Mungu mmoja anasema wachukie wanadamu wasio na imani kama yako, waue; halafu kuna Mungu mwingine anasema wapende, wasamehe, waombee, wavumilie, n.k., bila shaka hapa ndipo penye uwanja sahihi wa kutenganisha pande hizi mbili.

Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo akubariki ndugu msomaji.

Tafakari.

Hoji mambo

Chukua hatua.

******************
 Bado naendelea kungoja kwa hamu kubwa majibu ya maswali niliyouliza HAPA. Sijapata mtu wa kunijibu hadi sasa.

3 comments:

  1. Ukisoma 19:17 malaika alikuwa mmoja na 3 anzia 39 utaona kuwa malaika in mmoja aliyemletea maryam ubashiri ukija 42 hawakuwa wakibashiri wale malaika Bali wakimueleza maryam ya kuwa amebarikiwa.

    ReplyDelete
  2. Labda ungelejea Quran yako kwa utulivu na so kwa akili ya kihitikadi maana 10:92 na 28:40 zinaeleza maana moja.

    ReplyDelete
  3. Ukisoma 15 kuanzia 16 utaelewa 19 inaeleza kuwa kilichotandazwa ni ardhi.soma 2:2 kwa faida yako

    ReplyDelete